Sehemu ya tabia:

Jawabu: Amesema Mtume Sala na amani ziwe juu yake: "Muumini aliyekamilika kiimani ni yule mwenye tabia njema zaidi kuliko wengine". Kaipokea Tirmidhiy na Ahmad.

Jawabu: 1- Kwa sababu ni sababu ya kumpenda ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
2- Ni sababu ya kupendwa na viumbe.
3- Ni kitu kizito zaidi katika mizani.
4- Na malipo huzidishwa kwa sababu ya tabia njema.
5- Ni alama ya ukamilifu wa imani.

Jawabu: Kutoka katika Qur'ani tukufu, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Hakika hii Qur'ani inaongoa kwenye yale yaliyo nyooka kabisa}. [Suratul Israai: 9]. Na kutoka katika mafundisho ya Mtume: amesema Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hakika bila shaka nimetumwa ili nitimilize tabia njema". Imepokelewa na Ahmad.

Jawabu: Wema: Ni kumchunga Mwenyezi Mungu wakati wote, na kufanya mambo mazuri na kuwafanyia wema viumbe.
Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Hakika Mwenyezi Mungu ameandika wema juu ya kila kitu". Imepokelewa na Imamu Muslim
Miongoni mwa namna za wema:

Ni kufanya wema zaidi katika ibada za Mwenyezi Mungu Mtukufu, Na hilo linakuwa kwa kutakasa nia katika ibada zake.
-Kuwafanyia wema wazazi wawili, kwa kauli na vitendo.
-Kuwafanyia wema ndugu wa kuzaliwa tumbo moja na wale wa karibu katika ukoo.
-Kumfanyia wema jirani.
-Kuwafanyia wema mayatima na masikini.
-Kumfanyia wema aliyekukosea.
-Kufanya wema katika mazungumzo.
-Kufanya wema katika mijadala.
-Kumfanyia wema mnyama.

Jawabu: kinyume cha wema ni kukosea (kukwaza).
Miongoni mwa makosa:
Ni kuacha kutakasa nia katika ibada za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na kuwaasi wazazi wawili.
Kukata undugu.
Kuishi vibaya na majirani.
Kuacha kuwafanyia wema mayatima na masikini, na mengineyo katika aina za mazungumzo na matendo mabaya.

Jawabu:
1- Amana katika kuhifadhi haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Aina zake:
Amana katika utekelezaji wa ibada kama swala, zaka, swaumu, Hijja, na zinginezo katika zile alizozifaradhisha Mwenyezi Mungu juu yetu.
2- Amana katika kuhifadhi haki za viumbe:
Ikiwemo kuhifadhi heshima za watu.
Na mali zao.
Na damu zao.
Na siri zao, na yote ambayo watu wamekuamini.
Amesema Mwenyezi Mungu katika kutaja sifa za waliofaulu:
"Na wale ambao wanavitunza vitu vyote walivyoaminiwa navyo, na wanatekeleza ahadi zao zote." [Suratul Mu'minun: 8]

Jawabu: Ni hiyana, nayo maana yake ni kupoteza haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu na haki za watu.
Amesema Mtume Sala na amani ziwe juu yake:
"Alama za mnafiki ni tatu" Na akataja miongoni mwa hizo alaama "Na akiaminiwa anafanya hiyana" Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Jawabu: Ni kueleza kwa namna inayoendana na uhalisia wa tukio au kukieleza kitu kama kilivyo.
Na katika namna zake:

Ukweli wakati wa mazungumzo na watu.
Ukweli katika ahadi.
Ukweli katika kila kauli na kitendo.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake:
"Hakika ukweli unamuongoza mtu katika wema, na hakika wema unamuongoza mtu katika pepo, na hakika mtu husema kweli mpaka anakuwa mkweli" Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Jawabu: Ni uongo, nao ni kinyume cha uhakika, na miongoni mwake, ni kuwaongopea watu, kutotimiza ahadi, na kutoa ushahidi wa uongo.
Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- "Na Tahadharini sana na uongo! kwani uongo unapelekea katika uovu, na hakika uovu unampelekea mtu kuingia Motoni, na hatoacha mtu kuendelea kusema uongo, na kuutafuta uongo mpaka ataandikwa mbele ya Mwenyezi Mungu kuwa ni muongo". Wamekubaliana Bukhari na Muslim. Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Alama za mnafiki ni tatu" Na akataja miongoni mwake "Akizungumza husema uongo, na akitoa ahadi hatimizi". Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Jawabu: Kusubiri juu ya kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kusubiri kutoyaendea maasi.
-kusubiri juu ya makadirio ya Mwenyezi Mungu yaumizayo, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila hali.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na Mwenyezi Mungu anawapenda wenye kusubiri" [Surat Al Imrani: 146] Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Ajabu iliyoje ya jambo la muumini, hakika jambo lake lote ni kheri, na hakuna hilo kwa yeyote ila kwa muumini: akipatwa na jambo lenye kufurahisha anashukuru ikawa hilo ni kheri kwake, na akipatwa na madhara anasubiri likawa hilo ni kheri kwake." Imepokelewa na Imamu Muslim

Jawabu: Ni kutokuvumilia juu ya kumtii Mwenyezi Mungu, kutosubiri katika kuyaendea maasi, kulalamika na kuchukia makadirio kwa kuzungumza au vitendo vinavyoonyesha kutoridhishwa na makadirio.
Katika namna zake:

Kutamani kifo.
Kupiga mashavu.
Kuchana nguo.
Kusambaza nywele, kwa itikadi za kutoridhishwa na msiba uliotokea.
Kujiombea maangamivu.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake:
"Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu)." Kaipokea Tirmidhi na bin Majah

Jawabu: Ni watu kusaidizana wao kwa wao katika haki na mambo ya kheri.
Namna za kusaidizana:

* Kusaidizana katika kurudisha haki za watu.
* Kusaidizana katika kumzuia mwenye kudhulumu.
* Kusaidizana katika kukidhi mahitaji ya watu na masikini.
* Kusaidina katika kila kheri.
* Kutosaidizana katika madhambi na maudhi na uadui.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na saidianeni katika wema na uchamungu na wala msisaidiane katika madhambi na kufanya uovu,na muogopeni Mwenyezi Mungu kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu" [Suratul Maidah: 2] Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Muumini kwa muumini mwenzake ni kama jengo moja; linajiimarisha baadhi yake kwa baadhi" Wamekubaliana Bukhari na Muslim. Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake: "Muislamu ndugu yake ni muislamu, asimdhulumu na wala asimsaliti, na atakayekuwa katika shida ya ndugu yake, basi Mwenyezi Mungu naye atakuwa katika shida yake, na atakayetatua kwa muislamu matatizo, basi na Mwenyezi Mungu atamtatulia tatizo katika matatizo ya siku ya kiyama, na atakayemsitiri muislamu, Mwenyezi Mungu naye atamsitiri siku ya kiyama". Wamekubaliana Bukhari na Muslim.

Jawabu: 1- Kumuonea haya Mwenyezi Mungu: inakuwa kutomuasi mwenyezi mungu Mtukufu.
2- Kuwaonea haya watu: Na miongoni mwa haya ni kuacha maneno mabaya machafu, na kufunua uchi.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Imani iko zaidi ya sehemu sabini". "Au zaidi ya sitini" sehemu ya juu yake zaidi ni kauli ya (Laa ilaaha illa llaahu) Hapana Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na ya chini yake zaidi ni kuondoa maudhi njiani, na haya (aibu) ni sehemu katika imani." Imepokelewa na Imamu Muslim

Jawabu: -Kuwahurumia wazee na kuwaheshimu.
- Kuwahurumia wadogo na watoto.
- Kumhurumia masikini na mwenye shida.
-Kuwahurumia wanyama kwa kuwalisha na kutowaudhi.
Na katika hili ni kauli ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake:
"Mfano wa waumini katika kupendana kwao na kuhurumiana kwao na kufanyiana kwao upole, ni kama mfano wa kiwiliwili, kinapopata tabu kiungo kimoja vinaitana kwa ajili ya hicho kimoja viungo vyote kwa kukesha na maumivu" Wamekubaliana Bukhari na Muslim. Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni watu wa ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni." Imepokelewa na Abudaud na Tirmidhiy.

Jawabu: Ni kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na wale walioamini wanamapenzi makubwa kwa Mwenyezi Mungu" [Suratul Baqara: 165].
Kumpenda mtume - rehema na amani ziwe juu yake
Amesema:
"Namuapia yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake, hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake zaidi kuliko mtoto wake na mzazi wake". Imepokelewa na Al-Bukhaariy
Kuwapenda waumini, na kuwapendelea kheri kwao kama unavyoipendelea nafsi yako.
Amesema Mtume Sala na salamu ziwe juu yake:
"Hawezi kuwa na imani mmoja wenu mpaka ampendelee ndugu yake anachokipenda yeye katika nafsi yake" Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Jawabu: Ni ukunjufu wa uso, pamoja na furaha, tabasamu, upole na kudhihirisha furaha wakati wa kukutana na watu.
Nayo ni kinyume cha kukunja sura mbele za watu, kitu kinachoweza kuwafanya wakawanaye mbali.
Na katika faida zake, zimekuja hadithi nyingi, Kutoka kwa Abuu Dhari Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: alisema kuniambia mimi Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake: "Usidharau kabisa katika wema kitu chochote, hata kama ni kukutana na ndugu yako kwa uso mkunjufu." Imepokelewa na Imamu Muslim Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Tabasamu lako katika uso wa ndugu yako ni sadaka" Kaipokea Imamu Tirmidhiy

Jawabu: Ni kutamani neema ziwaondokee wengine, au kuchukia neema walizo pewa mtu.
Amesema Mtukufu:
"(Na ninaomba kinga kutokana) Na shari ya hasidi anapofanya husuda" [Suratul Falaq: 5]
Na Kutoka kwa Anasi bin Maliki Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, ya kwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake amesema: "Msichukiane, na wala msihusudiane, na wala msitengane, nakuweni waja wa Mwenyezi Mungu ndugu wamoja" Ameipokea Bukhari na Muslim.

Jawabu: Ni kumfanyia kejeli ndugu yako muislamu na kumdharau, na jambo hili halifai.
Amesema Mtukufu katika kulikemea hilo:
"Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo, wasitoke Waumini wanaume wakawacheza shere Waumini wanaume wengine, huenda akawa yule anayechezwa shere katika wao ni bora kuliko wale wenye kucheza shere, na wasitoke Waumini wa kike wakawacheza shere Waumini wakike wengine, kwani huenda yule anayechezwa shere miongoni mwao ni bora kuliko wale wenye kucheza shere. Wala msitiane dosari nyinyi kwa nyinyi, wala msiitane majina ambayo yanachukiwa na wenye kuitwa nayo, kwani ubaya wa sifa na jina ni utokaji nje ya maadili ya Dini, nao ni kucheza shere kwa njia ya dharau, kuaibisha kwa maneno au ishara na kupeana majina mabaya, baada ya kuwa mmeingia kwenye Uislamu na mmeufahamu. Na Asiyetubia na huku kuchezeana shere, kutiana dosari, na kuitana majina mabaya na utokaji nje wa maadili ya Dini, basi hao ndio watu waliozidhulumu nafsi zao kwa kuyatenda mambo haya yaliyokatazwa." [Suratul Hujurat: 11].

Jawabu: Ni mtu kutojiona yeye ni bora kwa watu, akawa hawadharau watu na wala haikatai haki.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na waja wa Arrahman mwingi wa rehema ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha" [Suratul Furqan: 63], Yaani: Wakiwa wanyenyekevu. -Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Na hajawahi kunyenyekea yeyote kwa ajili ya Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua" Imepokelewa na Imamu Muslim Na amesema Rehema na Amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu ameteremsha wahyi kwangu, yakuwa kuweni wanyenyekevu kiasi kwamba asifanye uovu mmoja wenu kwa mwingine, na asichupe mipaka mmoja wenu juu ya mwingine". Imepokelewa na Imamu Muslim

Jawabu: 1- Kufanya kiburi katika haki, nacho ni kuikataa haki na kutokuikubali.
2- Kuwafanyia kiburi watu, nako ni kuwadharau na kuwabeza.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Haingii peponi atakayekuwa moyoni mwake na chembe ndogo ya kiburi" Mtu mmoja akasema: Kuna mtu anapenda nguo yake kuwa nzuri, na viatu vyake kuwa vizuri (pia ni kiburi?) Akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri anapenda uzuri, kiburi: Ni kuikataa haki na kuwadharau watu" Imepokelewa na Imamu Muslim
-Kuibeza haki: Kuikataa.
-Kuwadharau watu: kuwabeza.
- Nguo nzuri na viatu vizuri hivi si katika kiburi.

Jawabu: Udanganyifu katika kuuza na kununua, nako ni kuficha aibu ya bidhaa.
-Udanganyifu katika kujifunza elimu, na mfano wake ni ghushi ya wanafunzi katika mitihani.
-Udanganyifu katika kauli kama kushuhudia uongo na kusema uongo.
- Kutotimiza unayoyasema na yale unayokubaliana na watu.
Na katika katazo la kudanganya, yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alipita katika gunia la chakula, akaingiza mkono wake ndani yake, vidole vyake vikapata unyevunyevu, akasema: "Ni nini hiki ewe muuza chakula?" Akasema: Kimenyeshewa na mvua ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Akasema: "Kwa nini usikiweke juu ili watu wakione? Yeyote mwenye kudanganya si miongoni mwangu" Imepokelewa na Imamu Muslim
Gunia: Ni mfuko wa chakula.

Jawabu: Ni kumsema ndugu yako muislamu kwa yale anayoyachukia akiwa hayupo katika mazungumzo.
Alisema Allah Mtukufu:
"Na wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi, Je yupo katika nyinyi anayependa kuila nyama ya nduguye aliyekufa? Mnalichukia hilo (bila shaka) Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kupokea toba, mwenye kurehemu" [Suratul Hujurat: 12].

Jawabu: Ni kuhamisha mazungumzo kati ya watu kwa ajili ya kuwavuruga.
Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Haingii peponi mfitinishaji" Imepokelewa na Imamu Muslim

Jawabu: Ni kuwa mzito katika kufanya mambo ya kheri na yale ambayo ni ya wajibu kwa mtu kuyafanya.
Na katika hayo ni kuwa mvivu katika kutekeleza majukumu.
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
"Hakika mbinu ya wanafiki hawa ni kumhadaa Mwenyezi Mungu kwa Imani wanayojionyesha nayo na ukafiri wanaouficha, kwa kudhani kuwa mbinu yao itafichikana kwa Mwenyezi Mungu, na hali ya kwamba Mwenyezi Mungu Ndiye Anayewahadaa na ni Mwenye kuwalipa malipo yanayofanana na vitendo vyao. Wanafiki hawa wanaposimama kutekeleza Swala, wanasimama kufanya hivyo kwa uvivu, wanakusudia, kwa kuswali kwao, kuonekana na kusikika. Na wao hawamtaji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, isipokuwa kumtaja kwa uchache". [Suratun Nisaa: 142]
Ni lazima kwa muumini kuacha uvivu, kuzubaa na kukaa, na aende mbio katika amali na achangamke na afanye bidii na juhudi katika maisha haya kwa yale yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Jawabu: 1- Hasira nzuri: Nayo ni ile inayokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu pale makafiri au wanafiki au wengineo wanapoyaendea maharamisho yake Mtukufu.
2- Hasira mbaya: Nayo ni hasira inayompelekea mtu kufanya au kuzungumza mambo yasiyofaa.
TIBA YA HASIRA MBAYA:

Udhu - kutawadha.
Kukaa ikiwa atakuwa kasimama, na kulala ikiwa atakuwa amekaa.
Ashikamane na usia wa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika hilo:
"Usikasirike"
Aidhibiti nafsi kutosukumwa na hasira akafanya maamuzi mabaya.
Kujikinga kwa Allah kutokana na shetani aliye laaniwa
Kunyamaza.

Jawabu: Ni kubaini na kutafuta aibu za watu pamoja na yale waliyoyasitiri.
Miongoni mwa aina zake za haramu:

- Kuchungulia uchi wa watu majumbani.
-Mtu kusikiliza mazungumzo ya watu bila ya wao kujua.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na wala msichunguzane". [Suratul Hujurat: 12].

Jawabu: Ubadhirifu: Ni kutumia mali bila sababu za msingi.
Na kinyume chake:
Ni Ubahili: Nako ni kuzuia kutoa katika jambo la lazima.
Na sahihi zaidi nikuwa katikati ya hayo, na muislamu anatakiwa kuwa mkarimu.
Amesema Allah Mtukufu:
"Na wale ambao wakitumia mali zao hawapitishi kipimo katika kutoa wala hawabani katika matumizi, na kutumia kwao huwa kuko kati na kati baina ya kupitisha kipimo na kubana." [Suratul Furqan: 67],

Jawabu: Uoga: Ni mtu kuogopa kitu ambacho hakitakiwa kuogopwa.
Mfano:
Kuogopa kusema ukweli na kukemea uovu.
Ushujaa:
Ni kujitosa katika ukweli, nao ni kama mfano wa kwenda mbele katika viwanja vya vita kwa ajili ya kuutetea uislamu na waislamu.
Na alikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akisema katika dua yake:
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na uoga". Na Amesema mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na Amani ziwe juu yake. "Muumini mwenye nguvu ni bora na anapendeka kwa Allah kuliko muumini dhaifu, na katika kila kheri" Imepokelewa na Imamu Muslim

Jawabu: Mfano kutoa laana na kutukana.
- Na mfano ni kauli ya fulani "We hayawani" Au mfano wake katika matamshi.
- Au kutaja nyuchi katika maneno mabaya na machafu.
- Na aliyakataza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake hayo yote, akasema: "Muumini si msemaji watu vibaya, wala mtoaji wa laana, wala muovu, wala mwenye kauli chafu" Kaipokea Tirmidhi na bin Majah.

Jawabu: 1- Kumuomba Mwenyezi Mungu amruzuku tabia njema na amsaidie juu ya hilo.
2- Kumchunga Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka, na kujua kuwa yeye anakujua, anakusikia na anakuona.
3- Kumbuka malipo ya tabia njema ni sababu ya kuingia peponi.
4- Kumbuka mwisho wa tabia mbaya, ni sababu ya kuingia motoni.
5- Kwamba tabia njema huleta mapenzi ya Mwenyezi Mungu na mapenzi ya viumbe wake, na tabia mbaya huleta ghadhabu za Mwenyezi Mungu na chuki za viumbe wake.
6- Kusoma historia ya Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake na kumuiga.
7- Kuambatana na watu wema na kujiepusha na kuambatana na watu waovu.